SHEREMBI AUNGA MKONO MATUMIZI YA VIFAA VYA TEHAMA BUKONGO
Автор: Ukerewe District Council
Загружено: 2025-04-10
Просмотров: 237
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Ndg. Emmanuel Sherembi amekabidhi Projector 1, Tv moja yenye ukubwa wa inch 55" aina ya LG na Computer tano za mezani zenye jumla ya shilingi Milioni 5 ili kuchoche ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi katika Shule ya Sekondari Bukongo Wilayani hapo.
Sherembi ameyatekeleza hayo Aprili 10, 2025 ikiwa ni ahadi aliyoitoa Septemba 29, 2023 wakati alipofanya ziara ya kikazi kukagua ujenzi wa miundombinu ya elimu shuleni hapo ambapo alifanya kikao na Walimu kuhimiza ufundishaji na utoaji wa hudima bora ya elimu kwa wanafunzi.
Kufuatia maombi ya Walimu na Wanafunzi waliyoyatoa kuhusu kusaidiwa vifaa vikiwepo Kompyuta, Projekta na Televisheni, Kwa wakati huo, Sherembi aliahidi kuitimiza ahadi hiyo mwezi Aprili 2025 kwa kununua vifaa hivyo ambavyo vitasaidia kuinua taaluma na kurahisisha utendaji kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Bukongo Mwl. Mwalubalo Bomba amesema vifaa hivyo vitasaidia kuwawezesha wanafunzi kupata rejea katika masomo yao, kujifunza masomo ya TEHAMA kwa vitendo ili kutulimiza ndoto zao.
Shule ya Sekondari Bukongo ni moja ya Shule kongwe iliyo na kidato cha 1 hadi cha 6, kwa hali ya sasa, Shule hiyo chini ya Utawala wa Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeongezewa miundombinu ya vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, mabweni umeme na maji hali ambayo imeendelea kuchochea maendeleo bora ya kielimu kwa wanafunzi waliopo hapo.
#sherembinakazi2025
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: