"HII SIYO NCHI INAYOTAFUTA DAMU" DKT NCHIMBI AUPIGA MARUFUKU WIMBO UNAOCHOCHEA CHUKI, AMTAJA LISSU
Автор: Millard Ayo
Загружено: 2025-04-25
Просмотров: 94753
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Emmanuel John Nchimbi amepiga marufuku wimbo unaobeza na kuchochea chuki dhidi ya vyama vya upinzani, akiagiza usitumiwe na wanaCCM popote, kwani wao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kuhamasisha upendo, umoja na mshikamano nchini.
Balozi Nchimbi alichukua hatua hiyo alipokuwa akihutubia umati mkubwa wa maelfu ya wananchi wa Mji wa Shirati, wilayani Rorya, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Obwele, leo Ijumaa tarehe 25 Aprili 2025, akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mara.
Akitumia simu yake kuucheza wimbo huo na kuwasikilizisha wananchi kupitia kipaza sauti alichokuwa anatumia kuhutubia, walisikika watu wakiimba wimbo unaofanana na ule wa dhidi ya Nduli Amin, huku wakiwa wamebadili maneno na kuweka mengine yanayolenga kubeza na kuchochea chuki dhidi ya vyama vya siasa vya upinzani nchini.
“Maneno haya katika wimbo huu ni maneno yanayojenga chuki. Hayajengi upendo. Napiga marufuku wimbo huu. Sisi wanaCCM tuna dhamana kubwa katika nchi hii. Lazima tuongoze kwa mfano. Tuunganishe watu. Tusiwe chanzo cha vurugu. CCM ndiyo baba na mama wa demokrasia nchini,” alisema Balozi Nchimbi kwa msisitizo.
Aidha, Balozi Nchimbi, mbali ya kutoa wito huo kwa wanaCCM, pia alitoa rai kwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani: “Wote, wanaCCM na vyama vya upinzani tujiepushe na kauli zinazochochea chuki na shari na vurugu. Hata tukimsikia kiongozi wa upinzani anatoa kauli za kuchochea, tuwatafute ndugu zake huko Singida, kuwa mshaurini ndugu yenu huko anakotupeleka siko.” Dkt Nchimbi
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: