AHSANTE KWA WEMA (OFFICIAL VIDEO) - Kwaya Kuu Mt. Cesilia Arusha, Tanzania
Автор: Verony Productions
Загружено: 2019-01-28
Просмотров: 177758
Available on all Platforms: https://album.link/tnzdgbjjdsnnx
Download or listen online: https://mdundo.com/song/2161752
Performers: Kwaya Kuu Mt. Cesilia Arusha, Tanzania
Producer: Verony Productions Ltd.
Composer: F.E. Single
Copyright ©Verony Productions Ltd.
1. Bwana alinitendea mambo makuu
Nilipoita jina lake aliniitikia
Alinitegemeza katika taabu zangu.
{Asante - kwa wema wako
Asante - kwa ukarimu
Asante kwa pendo lako nashukuru} * 2
2. Bwana ameniponya na magonjwa mengi
Pia amenikinga na ajali mbaya sana
Amenitoa katika mitego ya shetani.
3. Nimetafakari upendo wake Bwana
Kujivika ubinadamu na kufa msalabani
Ili nikombolewe utumwani wa shetani.
4. Ni mara nyingi sana nimetenda dhambi
Lakini Bwana Yesu hakunihukumu kwa dhambi
Hakuna kama Bwana yeye ni Mungu pekee.
5. Wema wake Mungu wangu hauna mwisho
Ameniandalia makao baada ya kifo
Masharti yake niwe nimetii amri za Mungu.
6. Enyi ndugu zangu mlio katika Kristu
Unganeni pamoja nami kumshukuru Mungu
Ni mema mengi sana yeye ametujalia.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: