WATANO WALIOPANGA KUFANYA VURUGU NA KUTAKA KUCHOMA MOTO WASHIKILIWA.
Автор: Revivalfmtz
Загружено: 2025-11-07
Просмотров: 61
Watu wa tano akiwemo mtumishi mmoja wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Tabora kitete wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kupanga kufanya vurugu pamoja na kutaka kuchoma moto sehemu mbalimbali ikiwemo ofisi na makazi ya viongozi wa serikali, vituo vya mafuta,yadi za mabasi zilizopo Tabora mjini siku ya uchaguzi mkuu octoba 29 mwaka huu.
Akitoa taarifa ya hali ya usalama ya kwa wajumbe wa kamati ya amani mkoa wa Tabora Mkuu wa mkoa huo Paul Matiko Chacha amesema kukamatwa kwa watu hao watano inatokana intelijensia kali ya vyombo vya ulinzi na usalama vya mkoa huo ambapo vilifanikiwa kuwabaini mapema watu hao kabla hawajatekeleza matukio hayo ambayo ni kinyume cha sheria za nchi.
Hata hivyo watuhumiwa hao watano ambao kwa sasa wote wapo mikononi mwa jeshi la polisi muda wowote kuanzia sasa watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: