Waziri Ummy Mwalimu Azungumzia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF na Bima ya Afya kwa wote
Автор: Mwangaza Online
Загружено: 2022-09-01
Просмотров: 631
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Bima ya Afya kwa wote ni suluhisho kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF kuendelea kuwepo na kutoa huduma bora kwa wanachama.
Waziri Ummy amesema kuwa mkakati uliopo sasa ni kuongeza idadi ya wanachama wa NHIF ili kuuwezesha Mfuko huo kuwa na watu walio na afya njema kuchangia wengine ambao wataugua ili waweze kupata tiba.
Waziri Ummy Mwalimu amesema asilimia kubwa ya wananchi waliojiunga kwa hiari katika Mfuko huo ni wagonjwa hivyo kuufanya Mfuko huo kutumia rasilimali nyingi kwa ajili ya matibabu ya wanachama wake ili hali wachangiaji bado wakiwa wachache hivyo kuwa na Bima ya Afya kwa wote kutauwezesha Mfuko huo kuwa na wanachama wengi na kuweza kutoa huduma bora zaidi na uhai mrefu kwa NHIF.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: