SITOWAVUMILIA WATENDAJI WAZEMBE KAZINI – DKT. BASHIRU
Автор: RS MOROGORO
Загружено: 2025-11-27
Просмотров: 2043
SITOWAVUMILIA WATENDAJI WAZEMBE KAZINI – DKT. BASHIRU
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Ally, amewataka watumishi wa umma hususan wa Wizara hiyo kuendelea kufanya kazi kwa kuwahudumia wafugaji inavyo paswa bila kuingiza masuala ya rushwa na baala yake wafanye kazi zao kwa uadilifu na ubunifu wa hali ya juu.
Balozi Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo Novemba 26, 2025 wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani Morogoro, ambapo ametembelea maeneo mbalimbali ya wafugaji na viwanda ili kujitambulisha na kujionea hali halisi ya uzalishaji katika sekta hiyo ya Mifugo na Uvuvi huku akiwathadhalisha watumishi wake.
“…Sitavumilia mtendaji wa mifugo mzembe, ambaye si mbunifu na wakati mwingine anayedai rushwa ili atoe huduma…” amesisitiza Dkt. Bashiru Ally.
Amesema, kutofanya kazi kwa ubunifu na kuendeleza tabia za kuda rushwa, wote watakaobainika na kadhia hiyo watachukuliwa hatua kali za kinidhamu na sheria ikiwemo kuwaondoa kazini. Amesisitiza watumishi wa kada hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii kuwatumikia wafugaji, huku akiwapongeza baadhi ya watendaji wanaotekeleza majukumu yao kwa weledi.
Aidha, Dkt. Bashiru amesema Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeelekeza kuainisha maeneo yote ya ufugaji yenye jumla ya hekta milioni 3.6 ili ifikapo mwaka 2030 tuwe na jumla ya hekta milioni 6 za ardhi ya ufugaji zilizobainishwa, zilizopangwa, zinazolindwa kisheria na zenye huduma zote zinazohitajika.
Sambamba na hayo, Dkt. Bashiru amewataka wafugaji kote nchini kuendelea kuwekeza katika mifugo hususan mbuzi na kondoo kwa kuwa wanyama hao kwa sasa wapo kwenye soko, kwani hadi sasa asilimia 62 ya mauzo yetu nchi za nje ni nyama za mbuzi na kondoo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, amesema wafugaji hasa wa Mkoa wa Morogoro ni lazima waondokane na uchungaji na kuingia kwenye ufugaji wa kisasa na wenye tija kwao na kwa taifa.
Amesema, hapo awali Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ilikuwa ikichangia milioni 40 katika sekta ya Mifugo na Uvuvi, ambapo kwa sasa sekta hiyo inachangia zaidi ya milioni 400 kutokana na utoaji wa Elimu kwa wafugaji kuhusu ufugaji wenye tija.
Mwisho.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: