MAMBO YANAYOATHIRI UBORA WA MBEGU ZA KIUME, NGONO ZEMBE NAYO YATAJWA
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2024-08-23
Просмотров: 10338
Wataalamu wa afya wametaja mambo sita ambayo mwanamume anapaswa kuwa makini nayo, ili kutoathiri ubora wa mbegu zake za kiume.
Ili binadamu akamilike, mwanamume anatakiwa kutoa chembeuzi ‘chromosome’ 23 na mwanamke chembeuzi 23 na kukamilisha Asidi Kiinideoksiribo ‘DNA’ 46.
DNA hizi hubeba vinasaba au jeni, yaani sehemu ambazo zinaamua tabia za kiumbe husika kama vile mwonekano, jinsia na yale yote kilichopokea kutoka kwa wazazi wake.
Lakini wasiwasi mkubwa hivi sasa ni kutokana na kushuka kwa kiwango na ubora wa mbegu za kiume, kutokana na tafiti zaidi ya 200 zilizofanyika duniani ukifikia nusu.
Mwanamume anaweza kuzaliwa vizuri akapata matatizo yakaathiri mbegu zake au akazaliwa tayari ana shida katika mbegu zake, ingawaje wanaopata matatizo baadaye idadi yao inatajwa kuongezeka.
Hili limetajwa kusababishwa na mambo mengi, hasa vyakula na mtindo wa maisha, athari zimejitokeza kwenye kiasi cha mbegu za uzazi anazotoa mwanamume, ubora wake na uwezo wake kuogelea katika majimaji ukeni kulifikia yai.
Mkuu wa kitengo cha upandikizaji mimba (IVF) Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk Matilda Ngarina anataja mambo ya kufuata na kuepukwa ili mwanamume awe na mbegu zilizo bora.
Dk Ngarina anasema mwanamume lazima ajue vitu vingapi vinaweza kuharibu ubora, akitaja wapo ambao huzaliwa wakiwa tayari na changamoto ya mbegu, ikiwemo shida za homoni, mfumo na wengine kupata athari baadaye na kuharibu ubora wa mbegu zinazozalishwa. Video kamili Youtube ya Mwananchi Digital.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: