RAIS SAMIA ATOA POLE KWA WAKRISTO WOTE BAADA YA PAPA FRANCIS KUAGA DUNIA
Автор: GB Global Media
Загружено: 22 апр. 2025 г.
Просмотров: 1 003 просмотра
GB GLOBAL MEDIA 🕊️ | April 21, 2025
Rais Samia atoa salamu za pole kufuatia kifo cha Papa Francis
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa *Dkt. Samia Suluhu Hassan*, kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, ametuma salamu za pole kwa waumini wa Dini ya Kikristo (Katoliki) kote duniani, kufuatia kifo cha Kiongozi wao, *Papa Francis*, aliyefariki dunia leo, Aprili 21, 2025 huko *Vatican*.
Kupitia mtandao wake wa *Instagram*, Rais Dkt. Samia aliandika 👇🏽
🕊️
"Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis. Katika kipindi chote cha miaka 12 akiwa Kiongozi wa Kanisa hilo, Papa Francisko ameishi maisha yake kama mwalimu na kiongozi aliyefundisha na kuhimiza ustawi na maendeleo ya watu pamoja na kudumisha amani."
"Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa waumini wote wa Kanisa Katoliki hapa nchini na duniani kote."
"Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi. Amina."
---
GB GLOBAL MEDIA
📰 Kwa taarifa sahihi na zinazogusa jamii.
📲 Tufuatilie kwa habari zaidi.

Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: