JINGU: WATOTO NI RASILIMALI YA TAIFA MALEZI MBADALA NI NGUZO KWA WANAOKOSA FURSA YA FAMILIA ASILI
Автор: #Ustawiwajamii DSM Digital
Загружено: 2025-12-01
Просмотров: 149
Katika kuendeleza juhudi za kuboresha ustawi wa jamii nchini, SOS Children’s Tanzania kwa ufadhili wa SOS Children’s Denmark kupitia Fairstart Foundation, imeendelea kutoa mafunzo maalumu ya malezi mbadala kwa njia ya mtandao.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021, jumla ya washiriki 120 wamehitimu mafunzo haya yanayodumu kwa miezi 6, yakihusisha:
Maafisa Ustawi wa Jamii
Maafisa Maendeleo ya Jamii
Walezi wa Makao
Chuo cha Ustawi
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Katika hotuba yake, Dkt. John Jingu, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, alisisitiza kuwa watoto ndio rasilimali muhimu ya taifa, na kwamba baadhi hukosa malezi ya familia kutokana na changamoto mbalimbali. Hivyo, mafunzo ya malezi mbadala yanabaki kuwa nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: