WATU SITA MBARONI KWA MAUAJI MOROGORO
Автор: ITV Tanzania
Загружено: 2026-01-22
Просмотров: 278
#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu sita kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya Sheya John Sweya (70), mkulima na mkazi wa Bwawa la Kihonda, wilayani Mvomero.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, SACP Alex Mkama, amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao huku upelelezi wa kina ukiendelea ili kubaini chanzo na mazingira kamili yaliyopelekea kifo cha mzee huyo.
Tukio hilo limeleta simanzi katika Kijiji cha Kihonda kutokana na ukimya na heshima aliyokuwa nayo marehemu enzi za uhai wake akiwa mkulima wa eneo hilo.
Jeshi la Polisi limeendelea kutoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama ili kukomesha vitendo vya ukatili na mauaji katika jamii.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: