HABARI PLUS TV

HABARI PLUS TV tunasukumwa na dhamira ya kupasha Habari kwa Jamii .Tunaahidi kutumia weledi wetu ili wewe mlaji wa habari zetu upate kile unachotegemea kwa ajili ya KUELIMIKA,KUBURUDIKA au kupata TAARIFA zitakazakusaidia katika kufanya maamuzi.

HABARI PLUS TV tunaheshimu uhuru wa kutoa maoni katika habari zetu mbalimbali tunazochapisha lakini hatutakuwa na uvumilivu kwa lugha za matusi,kejeli au kauli zisizo na staha iwe kwa mtazamaji au mhusika yeyote wa habari au taarifa iliyochapishwa.

Tukiongozwa na muongozo wa maudhui ya mtandanoni (Electronic and Postal Communications(Online Content)Regulations 2018) pamoja na sheria nyingine za nchi,tunaahidi kutochapisha taarifa au maoni ya mtu yenye mlengo wa kuchochea chuki dhidi mtu mwingine,taasisi au serikali hivyo maoni yenye chembechembe hizo yatafutwa bila kupewa taarifa kwa mtumaji na kama mtumaji huyo ataendelea na tabia hiyo ataondolewa.

Tunaomba ushirikiano wako ili tujenge jamii yenye upendo,amani na maadili mema.