CPT & TMCS TV

CPT ni chombo cha kusambaza habari njema.
Chombo hiki kinalenga kufanya uinjilishaji kupitia mtandao na sio chombo cha biashara wala chenye malengo ya kujitengenezea faida.Malengo makubwa ya CPT TV ni kuinjilisha kuelimisha na kuhabarisha jamii katika nyanja tofauti tofauti kikiongozwa na mafundisho ya Kanisa kuhusu jamii.
Pamoja na mambo mengine chombo hiki kitajikita katika malezi endelevu ya vijana hususani TMCS ambao kimsingi ndio wataalamu wajao na wadau wakubwa wa maendeleo.
Kupitia chombo hiki,tunalenga kuifikia jamii kwa kuwashirikisha sehemu ya machapisho yetu mbalimbali,ikiwa ni pamoja na mafundisho mbalimbali yanayotolewa na wataalamu wetu.