Carlos Kirimbai

Carlos R. W. Kirimbai ni mhudumu wa Injili ambaye ameitwa na Mungu kuufundisha Mwili wa Kristo.

Mungu alipomwiita aliongea naye kutoka kitabu cha Isaya 45: 13 akimwambia kuwa atamwinua katika haki, Naye atayanyoosha mapito yake yote. Ataujenga mji wa Mungu na kuwaweka huru watu wa Mungu waliyohamishwa.

Wakati Carlos akitamani kujua hili atalifanyaje Mungu akamwekea moyoni kulifundisha Neno la Mungu maana kwa maarifa mwenye haki anaokolewa.

Anachunga Kanisa la Manna Tabernacle Bible Church lililopo jijini Dar Es Salaam na anafanya seminar katika taasisi za elimu ya juu.

Anaufikia sana mwili wa Kristo kupitia mitandao ya jamii ikiwemo Youtube, Instagram, Facebook na Whatsapp.