PAPA FRANCIS AFARIKI AKIWA NA MIAKA 88 HUKO VATICAN
Автор: ITV Tanzania
Загружено: 21 апр. 2025 г.
Просмотров: 1 185 просмотров
#TANZIA: Papa Francis, mwenye umri wa miaka 88 amefariki dunia katika makazi yake huko Casa Santa Marta, Vatican.
Mwadhama, Kardinali Kevin Farrell, alitangaza kwa masikitiko kifo cha Baba Mtakatifu Francis, kwa kuandika "Ndugu wapendwa, kwa huzuni kubwa sina budi kutangaza kifo cha Baba Mtakatifu Francisko"
Papa Francis, jina lake halisi ni Jorge Mario Bergoglio, ambaye ni mzaliwa wa Argentina na ni Papa wa kwanza kuchaguliwa kutoka Amerika Kusini, Mara ya mwisho Papa alionekana hadharani Jumapili ya Pasaka akitoa baraka na ujumbe wa Pasaka.
Papa Francis, alichaguliwa kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki mwaka 2013, ameongoza Kanisa Katoliki kwa muda wa miaka 12.
Papa Francis alikuwa akipambana na changamoto za kiafya, ikiwa ni pamoja na nimonia na matatizo ya kupumua, yaliyomlazimu kulazwa katika Hospitali ya Gemelli mjini Roma.
Utaratibu Papa akifariki mazishi yanafanyika ndani ya siku 4-6 na baada ya siku 15 mikutano ya makardinali inafanyika ili kumchagua Papa mwingine.

Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: