Hii ndio hasara ya kumkataa Mungu. Hadithi ya kijana aliyemweka Mungu kwenye buti la gari
Автор: 7T7 MINISTRY
Загружено: 2022-12-12
Просмотров: 1013
Ilikuwa ni wikiendi ya furaha sana ambapo Kevi na marafiki zake walikubaliana kukutana na kuanza safari asubuhi ili kwenda kuvinjari ziwani. Walikuwa wameshawasiliana na mzazi wa Kevi na akawaruhusu kutumia gari la nyumbani kwao kwa ajili ya matembezi yao. Asubuhi ile walianza kupigiana simu na kuulizana ikiwa kila mmoja atafika kwa wakati ili wasichelewe kwenye matembezi yao. Kevi aliandaa nguo za matembezi pamoja na mavazi ya kuogelea, alihakikisha kuwa ameichaji simu yake vizuri kwa ajili ya kuchukua picha na video ili kuziweka mtandaoni, na pia hakusahau kuchukua vifaa vya dharura kwa ajili ya kujihami na lolote linaloweza kutokea wakiwa huko matembezini. Kwa sababu katika matembezi hayo vijana hawa walitaka kutumia gari ya akina kevi, basi kevi aliamka asubuhi zaidi ili kuhakikisha kuwa gari ipo katika hali salama kwa safari, aliangalia mafuta ikiwa yangewatosha kwenda na kurudi, aliangalia usalama wa tairi na vitu vingine vyote hadi alipojihakikishia kuwa gari ipo salama kwa safari ya kwenda na kurudi.
Wakati Kevi akiwa anafanya maandalizi yote hayo, mama yake alikuwa akimwangalia kwa ukaribu sana ili kuona ikiwa mwanae atakumbuka kila kitu katika safari yake.
Baada ya muda mfupi, rafiki zake Kevi walifika nyumbani wakiwa na shangwe za kwenda kufurahi. Kila mmoja akiwa katika muonekano tofauti na kila mtu akiwa amefanya maandalizi kwa upande wake. Ulipofika muda wa kuondoka, waliweka vyakula walivyoviandaa kwenye buti, na kisha wao wakaingia kwenye gari. Kabla ya kuondoka, mmoja wao akawakumbusha rafiki zake kuwa walikuwa wamesahau trei ya mayai ambayo walitaka wakaifanyie majaribio ya kuchemsha kwenye chemichemi iliyokuwa ikitoa maji ya moto. Hivyo Kevi akakimbia kwenda kuichukua trei ile na kuiweka kwenye buti la gari.
Alipotaka kuanza safari, mama akamwambia Kevi. “mwanangu, Katika safari yako naona umejitahidi kuwa makini kukumbuka kila kitu, lakini kuna kitu kimoja umekisahau”. Kevi akamuuliza mama yake, “ni kitu gani hicho nilichokisahau mama?”. mama yake akamwambia, “umesahau kumwambia Mungu aende pamoja nanyi katika safari yenu.” Baada ya kusikia hivyo, kevi hakufurahishwa na maneno ya mama yake, maana alidhani kuwa mama ataongea jambo lingine la maana zaidi kumbe anaongea habari za kutembea pamoja na Mungu. Basi kevi akasema, “mama wewe mwenyewe unaona kuwa gari limejaa, na hakuna siti yoyote iliyobaki hata kwa ajili ya panya mdogo. Sasa huyo Mungu wako atakaa wapi? Labda akae kwenye buti, maana huko ndio kumebaki na nafasi ya kutosha.” Baada ya kuongea maneno hayo kevi akakimbia na kuingia ndani ya gari, kisha wakaanza safari.
Safari yao ilikuwa nzuri. Marafiki hawa walipiga stori na kufurahi pamoja tangu mwanzo wa safari yao. Waliweka muziki mzito kwenye gari, walikuwa wakisafiri huku wakiendelea kunywa na kufurahi, na kama unavyojua mambo ya vijana wanapokuwa pamoja namna hiyo, walikuwa katika spidi kali mno.
Baada ya mwendo mrefu walifika katika eneo lililokuwa na kona kali, na kwa sababu walikuwa kwenye mwendo mkali, gari lilimshinda kevi na kupitiliza kwenye makorongo yaliyokuwa nje ya barabara. Kwa sababu makorongo yalikuwa marefu na yenye mawe mawe, gari lilibiringita na kujigongagonga hadi kufika chini kabisa ya korongo.
Baada ya dakika chache watu wakaja kwa ajili ya kuwaokoa. Lakini kwa bahati mbaya, hakuna hata mmoja wao aliyetoka akiwa mzima. Wote walifariki pale pale. Gari lao lilikuwa limeharibiwa kiasi kwamba ilikuwa vigumu kujua kuwa lilikuwa aina gani ya gari. Lakini walipoangalia upande wa nyuma wa gari, waliona kuwa gari haikudhurika. Na walipofungua buti la gari, kila mmoja aliyefika pale alishangaa kuona kile walichokiona.
Subscribe / @7t7ministryenglish24 ili upate kubarikiwa na Bible quizes za kiingereza
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: