Usijidharau. Hii ndio thamani yako halisi. Hadithi fupi yenye funzo
Автор: 7T7 MINISTRY
Загружено: 2022-12-22
Просмотров: 743
Kijana mdogo alimuuliza baba yake “maisha yangu yana thamani kiasi gani?”
Baba yake alichukua jiwe na kumpa mtoto wake kisha akamwambia kuwa aende nalo sokoni akaliuze lile jiwe. Kama akitokea mtu akamuuliza bei ya lile jiwe, asijibu chochote ila aoneshe vidole viwili.
Yule kijana akaenda sokoni kuuza lile jiwe. Baada ya muda kidogo akatokea mwanamke mmoja aliyevutiwa na lile jiwe. Akasema kuwa anataka kwenda kupamba lile jiwe sebuleni kwake maana limemvutia sana. Alipomuuliza kijana bei ya lile jiwe, kijana alifanya kama alivyoambiwa na baba yake, akaonesha vidole viwili na wala hakusema neno lolote. Yule mwanamke akasema, “sawa nitanunua kwa shilingi elfu mbili.”
Kijana akarudi nyumbani haraka na kumwambia baba yake kuwa kuna mwanamke anataka kununua lile jiwe kwa shilingi elfu mbili. Baba yake akamwambia. “kabla hujauza jiwe hilo kwa huyo mwanamke, nenda kwenye jumba la makumbusho halafu kawaoneshe jiwe hilo. Wakikuuliza bei yake usiseme kitu chochote ila onesha vidole viwili kama ulivyofanya kwa huyo mwanamke, baada ya hapo uje unipe jibu.”
Kijana akatoka mbio kwenda kwenye jumba la makumbusho na kumkuta afisa manunuzi wa jumba la makumbusho. Baada ya kuliona jiwe lile, afisa manunuzi akatamani kulinunua ili aliweke kwenye makumbusho maana lilikuwa na mvuto wa pekee. Akamuuliza yule kijana bei ya lile jiwe. Kijana alifanya kama alivyoambiwa na bababa yake, akaonesha vidole viwili. Yule afisa manunuzi akamwambia sawa, nitakulipa laki mbili.
Kijana akiwa ameshikwa na mshangao akatoka kwenye jumba la makumbusho na kukimbia haraka kwenda kwa baba yake na kumwambia kuwa afisa manunuzi wa jumba la makumbusho alikuwa tayari kununua lile jiwe kwa pesa nyingi zaidi kuliko yule mwanamke aliyekutana nae sokoni. Baba yake akamwambia. “kabla hujauza hilo jiwe kwenye jumba la makumbusho, nenda kwa sonara na umuoneshe hilo jiwe. Akikuuliza bei yake usiseme kitu chochote ila onesha vidole viwili kama ulivyofanya kwenye jumba la makumbusho, baada ya hapo uje unipe jibu.”
Kijana akiwa na hamu ya kutaka kujua sonara atasemaje, alikimbia haraka na kwenda kumuonesha lile jiwe. Baada ya kuliona lile jiwe, sonara alishangaa sana na kumwambia kijana. “Hiki ni kito cha thamani sana. Nimekitafuta muda mrefu bila mafanikio. Sasa nitanunua hili jiwe kwa bei yoyote utakayonitajia. Utaniuzia bei gani?” kijana akaonesha vidole viwili bila kuongea neno lolote kama alivyoelekezwa na baba yake. Sonara akasema, sawa hakuna shida, nitakulipa hiyo milioni ishirini. Kijana akarudi kwa baba yake akiwa haamini kuona kile anachokishuhudia. Akamwambia baba yake kuwa sonara alikuwa tayari kununua lile jiwe kwa milioni ishirini.
Baba akamwambia mtoto wake, “Mwanangu, wewe ni kama hilo jiwe la thamani. Lakini kama ukiangukia katika mikono ya mtu asiyejua thamani yako, atakuchukulia poa tu na kudhani kuwa unafaa kupambwa sebuleni kama yule mwanamke alivyofanya. Kama utaangukia katika mikono ya mtu anayetambua thamani yako nusunusu, basi atakuchukua ili ukapambe makumbusho kama afisa manunuzi wa jumba la makumbusho. Lakini kama utafika katika mikono ya mtu ambaye anatambua thamani yako. Kama utakutana na mtu aliyehangaika kupata mtu kama wewe bila mafanikio, basi ni wazi kuwa mtu huyo atakuthamini kama ambavyo sonara alilithamini hili jiwe.”
Usihangaike kwa ajili ya watu wanaoidharau thamani yako. Hao ni kama yule mwanamke aliyedhani jiwe hili la thamani ni kwa ajili ya mapambo tu. Ujinga wao na kutokujua kwao kumewakosesha fursa ya kumiliki utajiri mkubwa ambao umekuja hadi katika mikono yao. Muonee huruma kila anayekudharau maana anafanya hivyo kwa hasara yake mwenyewe. Usihangaike kumthibitishia kuwa wewe ni wa thamani, maana kamwe hawezi kukubali kwa sababu ya uelewa wake mdogo. Atakuja kuelewa vizuri siku atakayokukuta umekaa kwenye kabati zuri kuliko makabati yote ya sonara. Siku moja atakuja kukuona ukiwa umevaliwa shingoni mwa wafalme na watu wenye heshima duniani, wakati yeye akiwa anaendelea kukanyaga vumbi na kupigwa na jua. Wakati huo ataanza kujigamba kwa watu kuwa anakufahamu na wewe unamfahamu. Ataanza kusimulia hadithi za zamani. Lakini hiyo yote itakuwa historia baada ya yeye kuchelewa sana.
Kuna faida kubwa sana ya kukaa kwenye mikono ya sonara huyu atakayekuheshimisha.
Angalia video hii ili ufahamu faida kubwa za kukaa kwa sonara huyu.
Usisahau kusabskraib na kubonyeza alama ya kengele ili uweze kupata mafundisho mengi zaidi kutoka seventiseven ministry.
Subscribe / @7t7ministryenglish24 ili upate kubarikiwa na Bible quizes za kiingereza
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: