Ziara ya Dkt Homera Lusewa yaandoka na watumishi wawili kwa utendaji mbovu.
Автор: Site Tv Online
Загружено: 2026-01-17
Просмотров: 221
DKT HOMERA AAGIZA WATUMISHI WAWILI LUSEWA KUHAMISHWA KWA UTENDAJI MBOVU.
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mhe Dkt Juma Zuberi Homera amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kuwahamisha watumishi wawili wa kata ya Lusewa ambayo ipo katika wilaya ya Namtumbo kufuatia hali ya utendaji kazi mbovu.
Maagizo hayo ameyatoa wakati anakabidhi gari ya kubeba wagonjwa katika kituo cha afya cha kata ya Lusewa ambapo wananchi wa kata hiyo walitoa malalamiko ya mganga mkuu wa kituo cha afya cha kata ya Lusewa ambaye ametajwa kuwatoza wajawazito faini ya shilingi 50,000 pale wanapochelewa kwenda kuanza kliniki.
Pia mtumishi mwingine ni afisa mtendaji wa kata ya Lusewa ambaye ameshindwa kutekeleza majukumu yake ikiwemo kusimamia ufanisi wa miradi ya kata hiyo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: