LITANIA, NADHIRI ZA DAIMA WATAWA WA MASHIRIKA WA JIMBO LA IRINGA
Автор: JIMBO KATOLIKI IRINGA ONLINE TV
Загружено: 2025-12-11
Просмотров: 1121
Mhashamu Baba Askofu Romanus Mihali Askofu wa Jimbo La Iringa ametoa nadhiri za Daima Kwa watawa wa Kike Na Wakiume Kwa Mashirika Ya Theresia wa mtoto yesu Na Moyo safi wa Bikira Maria Imakulata (SCIM) wa Jimbo la Iringa
Askofu Mihali amefanya adhimisho la Misa Takatifu ya nadhiri za daima Desemba 08 2025 katika parokia ya Moyo mtakatifu wa Yesu - Tosamaganga Jimboni Iringa kwa mashirika hayo huku watawa wakike waliopokea nadhiri hizo wakiwa 19 kutoka shirika la Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu na watawa wa kiume watatu kutoka shirika la Moyo safi wa Bikira Maria Imakulata.
Katika homilia yake amewataka watawa kujitoa kumtumikia Mungu bila kujibakiza na watambue kuwa wito wa Mungu ni neema hivyo yafaa kumtumtukuza Mungu na kumpa sifa.
Katika kuelekea sherehe za Maadhimisho ya siku ya uhuru Nchini Tanzania askofu Mihali aliwataka waamini kuiombea Nchi na kuikabidhi kwa Mama Bikira maria ili nchi iwe ya haki na amani.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: