BASHUNGWA ATOA MASAA MATATU KUREJESHWA MAWASILIANO YA BARABARA YA MTWARA - MASASI ILIYOKATIKA
Автор: Wizara ya Ujenzi
Загружено: 2024-03-04
Просмотров: 47263
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameelekeza Wakala wa Barabara (TANROADS) kuhakikisha wanarejesha mawasiliano ya barabara iliyokatika eneo la Maili Mbili katika barabara ya Mtwara-Mingoyo-Masasi ndani ya masaa matatu mara baada ya Daraja kusombwa na maji katka eneo hilo.
Bashungwa ametoa agizo hilo tarehe 04 Machi, 2024 Wilayani Masasi akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Deo Ndejembi, alipofika hapo kujionea adha ya watumiaji wa barabara hiyo waliokwama tangu majira ya asubuhi kutokana na kukatika kwa miundombinu hiyo iliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha usiku wa jana.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: