Vilio vyaibuka Lucky Vicent, Wazazi na wanafunzi washindwa kuvumilia
Автор: Dar24 Media
Загружено: 2017-08-19
Просмотров: 110014
Watoto watatu wa Shule ya Msingi Lucky Vincent waliokuwa majeruhi wa ajali iliyotokea Arusha na kwenda kutibiwa nchini Marekani, wamewasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mjini Moshi na kupokelewa na mamia ya Watanzania.
Doreen, Sadia na Wilson walikuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Mercy, Sioux City nchini Marekani wamewasili kwa ndege ya Samaritan's Purse wakitokea nchini humo baada ya kupata nafuu.
Watoto hao ni miongoni mwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent walionusurika kifo katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Arusha mwezi Mei mwaka huu, ambapo inakadiriwa idadi ya waliopoteza maisha ni 33 ikijumuisha wanafunzi na walimu waliokuwa katika gari hilo.
--
Dar24 ni chanzo namba moja cha habari kwa watanzania mahali popote walipo duniani. Kwa habari za uhakika kutoka nyanja mbali mbali tembelea www.dar24.com
#Dar24 #Dar24Media
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: