UCHAGUZI MKUU 2025 -“HATUENDI VITANI ,TUNALINDA AMANI” IGP WAMBURA
Автор: TZA MEDIA HUB
Загружено: 2025-08-13
Просмотров: 34
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amesema kuwa Jeshi la Polisi halijiandai kwa ajili ya vita, bali kwa ajili ya kusimamia amani, utulivu, na usalama wa Taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi unaofanyika katika Shule ya Polisi Moshi, IGP Wambura amesema maandalizi ya jeshi la polisi kuelekea uchaguzi mkuu yanaangazia mikakati madhubuti ya kuhakikisha wananchi wanashiriki uchaguzi katika mazingira salama.
“Kwetu Jeshi la Polisi, tunajipanga, tuna mkakati, tunakutana, tunaongea, tunajadili... hatuendi vitani. Tunakwenda kusimamia amani, tunakwenda kusimamia utulivu wa taifa letu kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu,” alisema IGP Wambura huku akishangiliwa na maofisa waliokuwepo ukumbini.
IGP Wambura amesisitiza kuwa mafanikio ya uchaguzi wowote hutegemea maandalizi ya mapema na ushirikiano wa wadau mbalimbali, akiwemo mwananchi wa kawaida, vyombo vya usalama, tume ya uchaguzi, na vyama vya siasa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, mgeni rasmi katika mkutano huo, amesisitiza mashirikiano baina ya jeshi la polisi ,wananchi na tume ya uchaguzi na kwamba Serikali haitavumilia vitendo vyovyote vya kuvuruga utulivu wa nchi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: