NENO LA SIKU | Yohana 7 | Maombi Ya Kushinda Wanaotaka Kukuua | Isaac Javan
Автор: Neno La Siku
Загружено: 2024-10-15
Просмотров: 4086
Leo tunasoma kitabu cha Yohana sura ya saba na tunaenda kufanya maombi ya kushinda wanaotaka kukuua. Moja kati ya kazi ambazo shetani anafanya kwenye dunia hii, ni pamoja na kuua watu wasiotakiwa kufa, au kuua watu ambao muda wao wa kufa haujafika.
Na moja kati ya silaha anazotumia, ni ushirikina. Wachawi wanatumika kama vyombo vya kutekeleza mauaji ya watu. Si kila mtu unayesikia amekufa amekufa kwa sababu muda wake umefika. Wengi wanauliwa na shetani kwa nguvu za kichawi. Lakini Mungu ametupa nafasi ya kuwashinda siku ya leo, kwa kupitia maombi haya.
Nami nakuombea, kwamba katika maombi ya leo ukapate ushindi. Mahali popote ambapo shetani alikusudia mabaya, BWANA akushindie na kuyageuza yote kuwa mema. Mahali popote ulipoandikiwa mauti, damu ya YESU itangaze na kuachilia uzima kwa ajili yako. Ukaishi siku nyingi na kuuona ukuu na uaminifu wa Mungu kwenye maisha yako. Ameen!
Isaac Javan
+255 745 76 45 72
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: