HERI MTU YULE AMCHAYE BWANA - ST. RITA RUAKA CHOIR
Автор: ST. RITA RUAKA CHOIR
Загружено: 2025-07-01
Просмотров: 11237
Kumcha Bwana kunaleta baraka nyingi na neema. Mjaribu Mungu kwa kumcha uone anavyofanya mambo.
HERI MTU YULE AMCHAYE BWANA Na Chris Oyier
(Heri mtu Yule amchaye Bwana),x2
(Apendezwaye sana, apendezwaye sana na maagizo yake.)x2
(Sop & Alto): Aleluya heri mtu Yule, amchaye Bwana; apendezwaye sana na maagizo yake.
(Tenor &Bass): Wazao wake watakuwa hodari, duniani; kizazi cha wenye adili, kitabarikiwa.
(Sop & Alto): Nyumbani mwake mna utajiri, utajiri na mali; na haki yake yakaa milele milele.
(Tenor &Bass): Nuru huwazukia wenye adili, gizani; ana fadhili na huruma, na haki.
(Sop & Alto): Heri atendaye fadhili, na kukopesha; atengenezaye mambo yake kwa adili.
(Tenor &Bass): Kwa maana hataondoshwa kamwe, mwenye haki; mwenye haki atakumbukwa, milele.
(Sop & Alto): Hataogopa habari mbaya, moyo wake; u imara ukimtumaini Bwana.
(Sop & Alto): Hataogopa habari mbaya, moyo wake; u imara ukimtumaini Bwana.
Tenor &Bass): Moyo wake umethibitika, hataogopa; hata awaone watesi, wake wameshindwa.
Hitimisho
(Wote): Amekirimu na kuwapa masikini, haki yake yakaa milele.
(Sop): aa aa aa aa, aa aa aa aa.
(Alto): uu uu uu uu, uu uu uu uu.
(Tenor): Amekirimu na kuwapa masikini, haki yake yakaa milele.
(Bass): oh oh oh oh, oh oh oh oh.
(Wote): Pembe yake itatukuzwa, itatukuzwa kwa utukufu.
To request the music sheet, email us at [email protected]
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: