MARAIS WETU WAMEJIZATITI KUWAPOKEA CHW KUHAKIKISHA TAIFA LINASONGA MBELE
Автор: ELIMU YA AFYA ONLINE TV
Загружено: 2024-09-03
Просмотров: 236
“Tumekuja kuwekeza kwa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika kubadilisha mwenendo wa utoaji wa huduma, lazima tuwafundishe, tuwawezeshe, na tuhakikishe wanapata Stahiki nzuri ili watusaidie, kwa kweli Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kule Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi wamejizatiti katika mstari wa mbele kulipeleka gurudumu la afya maana yake matatizo yote yanaanzia kulekule kwa jamii na kuyamaliza kulekule kwa jamii kupitia Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii”
Dkt. Salim Slim Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati Akizungumza katika Kikao Kazi cha Kuandaa Mpango wa Kuharakisha Utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii nchini kilichoratibiwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa la Afrika (Africa CDC) pamoja na Wadau wengine leo tarehe 3, Septemba, 2024 Jijini Dar es Salam.
Pata elimu kuhusu masuala yote ya afya kupitia Channel hii. Mafunzo yote yanatolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara ya Kinga, Kitengo Cha Elimu ya Afya kwa Umma kwa kushirikiana na wadau mbali mbali
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: