KILICHOWAKUTA WAFUGAJI MNADANI
Автор: Daily News Digital
Загружено: 2025-12-23
Просмотров: 2157
SIKONGE, Tabora: MIFUGO inayosafirishwa au kuuzwa katika minada hukumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa maji na chakula wakati wa safari, kupata majeraha kutokana na msongamano na usafirishaji usiozingatia ustawi wa mnyama, kuenea kwa magonjwa yanayotokana na kuchanganywa kwa mifugo kutoka maeneo tofauti, kuathiriwa na joto kali pamoja na hatari ya vifo njiani, hali inayosababisha hasara kwa wafugaji na kudhoofisha biashara ya mifugo kwa ujumla.
Kufuatia hali hiyo, wataalam wa mifugo kutoka Kituo cha Mifugo Kanda ya Magharibi cha Wizara ya Mifugo wametoa mafunzo kwa wafugaji kuhusu usalama na ustawi wa mifugo pamoja na mbinu bora za uendeshaji wa biashara ya mifugo, mafunzo ambayo yalitolewa kwa wafugaji wakiwa katika eneo la mnada wilayani Sikonge mkoani Tabora, yakilenga kupunguza vifo, magonjwa na majeraha ya mifugo sambamba na kuongeza tija na thamani ya biashara hiyo.
Follow us on:
FACEBOOK;
SpotiLeo: / spotileo-176. .
HabariLeo: / habarileo
DailyNews: / dailynewstz
INSTAGRAM;
HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig...
SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid...
TWITTER;
Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: