WANNE WAFARIKI KWA KUANGUKIWA NA UKUTA KANISANI, 12 WALAZWA DODOMA
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2025-12-25
Просмотров: 580
Watu wanne wamepoteza maisha na wengine 17 kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na ukuta wa Kanisa la Anglikana, Dodoma ulianguka wakati waumini wakiwa ndani.
Tukio hilo limetokea jioni ya Jumatano Desemba 23, 2025 katika Kijiji cha Wiliko Kata ya Mlowa Wilaya ya Chamwino ambapo Mwananchi ilipomtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa Dodoma, Gallus Hyera kuthibitisha taarifa hiyo hakupatikana kwani mara kadhaa simu yake ilipopigiwa haikuwa hewani.
Askofu wa Kanisa hilo Dayosisi ya Central Tanganyika, Dk Dickson Chilongani ametangaza michango kwa makanisa yote kwa ajili ya kuwahudumia majeruhi hao.
Naye, Mwenyekiti wa Kijiji cha Wiliko Gabriel Mika amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kueleza sababu kwamba ilitokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali ambapo watu 17 walijeruhiwa na wengine watano kupatiwa matibabu katika zahanati ya kijijini hapo, huku 12 wakipelekwa hospitali ya mjini Dodoma.
"Ni kweli amefariki mwanaume mmoja na Wanawake watatu wote ni watu wazima wa kijijini kwangu, hapa nipo msibani," amesema Mika.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti, majeruhi walikuwa 17 ambapo baada ya wawili kupoteza maisha, walibaki watano wanaoendelea kutibiwa Hospitali ya rufaa ya Dodoma.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Dk Ernest Ibenzi amekiri kupokea majeruhi 12 wa tukio hilo ambao amesema wanaendelea na matibabu.
Ufafanuzi matumizi ya picha na jina la kanisa
Leo Desemba 25, 2025 kwenye ukurasa wetu wa Instagram tumechapisha taarifa kuhusu ukuta wa Kanisa la Kanisa la Reality Of Christ Dodoma (ROC) Dodoma, kuanguka na kuua watu wanne na kujeruhi wengine 17.
Usahihi ni kwamba, ukuta ulioanguka na kuua watu wanne na kujeruhi wengine 17 ni wa Kanisa la Anglikana Dodoma na siyo Kanisa la Reality Of Christ Dodoma (ROC) kama ilivyoonekana kwenye habari hiyo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: