MCHUNGAJI AUWAWA KWA KUPIGWA AKIDAIWA MKUMLOGA KATEKISTA WA KATOLIKI HADI KUFA..
Автор: WATETEZI TV
Загружено: 2025-04-19
Просмотров: 939
Mchungaji Goden James Ngumbwike (66) wa kanisa la Pentecoste Evangelical Fellowship Of Africa lililopo Iganjo, amefariki dunia baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali akiwa nyumbani kwake wakimtuhumu kumloga hadi kufa jirani yake Katekista wa kanisa Katoliki Fadhili Komba, wa kigango cha Mwansekwa jimbo kuu katoliki la Mbeya na Mkazi wa mtaa Mwafute kata ya Ilemi Jijini Mbeya.
Tukio la kupigwa hadi kufa kwa mchungaji Ngumbwike Limefanywa Na Wananchi April 17 ,2025 majira ya mchana Akiwa Nyumbani Kwake Mtaa Wa Mwafute Kata Ya Ilemi Jijini Mbeya, Wakimutuhumu Mchungaji kuwa Ndiye Mhusika Mkuu Wa Kifo Cha Jirani yake Katekista Fadhili Komba Ambaye Alifariki Dunia April 15 Mwaka huu, Baada Ya Kuugua Muda Wa Miezi Mitano Na Kwamba Maradhi Yalimuanza Baada Mgogoro Wa Mpaka Kati Ya Hao Wawili.
Wakizugumza Na Watetezi Tv Viongozi hao Kabla Ya Tukio Hilo Viongozi Wa Mtaa Wa Mwafute Pamoja Na Kimila Walishawahi Kulizungumzia Na Kumtaka Katekista Aombe Radhi, Na Licha Ya Kufanya Hivyo Lakini Bado Aliendelea Kuumwa Hadi Umauti Unampata Kama Ambavyo Viongozi Wanazungumzia Sakata Hilo.
Viongozi Hao wameongeza kuwa Licha Kuwa Serikali kutoamini uchawi, wanakemea kitendo cha wananchi kujichukuliwa sheria mkononi, na sababu zilizofanya wananchi kuamini kuwa katekista huyo kalogwa ni baada ya mchungaji huyo kukubali kuombwa msamaha lakini pia na kauli ambazo aliwahi kuzitoa dhidi ya katekista ambaye ni jirani yake.
Juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi zinaeleendelea ili kuzungumziA suala hilo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: