Jinsi ya kupata Pasipoti ya kusafiria kupitia mtandaoni.
Автор: Nukta TV
Загружено: 2026-01-20
Просмотров: 12
Jinsi ya kupata Pasipoti ya kusafiria kupitia mtandaoni.
Huenda ukawa una ndoto za kusafiri kwenda nje ya Tanzania na hujui ni jinsi gani unaweza kupata pasipoti ya kusafiria. Ndoto hizo yawezekana ni kwa ajili ya shughuli za kibiashara, kimasomo au hata kwa ajili ya kutalii.
Pasipoti ya kusafiria ni hati rasmi ya utambulisho wa kimataifa inayotolewa na Serikali ya Taifa fulani kwa raia wake, inayomruhusu kusafiri kwenda nje ya nchi na kurejea nyumbani kisheria.
Utambulisho huu unamsaidia raia kufanya shughuli rasmi zilizompeleka mahali husika bila kizuizi na hata kupatiwa msaada pale inapohitajika.
Kwa Tanzania, pasipoti hutolewa na Idara ya Uhamiaji na Mchakato wa maombi yake unanzia kwenye tovuti ya idara hiyo, ambayo ni www.immigration.go.tz, ambapo ukishaingia katika tovuti hiyo unatakiwa kwenda katika kipengele cha huduma za uhamiaji yaani ‘eservice’.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: