BASHE KUZINDUA KIWANDA CHA KOROSHO NEWALA
Автор: Daily News Digital
Загружено: 2024-09-30
Просмотров: 692
NEWALA, Mtwara: WAZIRI wa Kilimo, Husein Bashe kesho Oktoba Mosi anatarajiwa kuzindua Kiwanda cha kubangua Korosho kinachomilikiwa na Chama Kikuu Cha Ushirika, Tandahimba na Newala (TANECU) kilichojengwa kwa gharama ya sh bilioni 3.4 katika Kijiji cha Mmovo Kitangari wilayani Newala mkoani Mtwara.
Meneja Mkuu wa TANECU, Mohamed Mwinguki amesema mpango wa chama hicho ni kujenga viwanda kama hivyo 20 na kila kiwanda kiwe na uwezo wa kubangua Korosho ghafi tani 3,500 kwa mwaka.
Kwa upande wake Mrajisi na Mtendaji Mkuu Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) Dk. Benson Ndiege amesema kiwanda hicho kimejengwa kwa nguvu ya wakulima ambao wanafanya kazi pamoja na chama kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala huku akitoa wito kwa wakulima na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushiriki uzinduzi huo.
Follow us on:
FACEBOOK;
SpotiLeo: / spotileo-176. .
HabariLeo: / habarileo
DailyNews: / dailynewstz
INSTAGRAM;
HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig...
SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid...
TWITTER;
Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: