HOTUBA YA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA MHE. DKT. JUMA ZUBERI HOMERA.
Автор: RITA Tanzania
Загружено: 2025-12-01
Просмотров: 294
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Juma Zuberi Homera amewataka wajumbe wa Bodi za Wadhamini nchini kuzingatia Sheria, kanuni na katiba zao wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kulinda haki na kusimamia rasilimali za taasisi zao kwa maslahi mapana ya jamii husika.
Mhe. Dkt. Homera ameyasema hayo wakati akifungua kikao cha Wajumbe wa Bodi za Wadhamini wa mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida, Iringa na Manyara kilichofanyika Novemba 27, 2025 mkoani Dodoma.
Pia, Mhe. Dkt. Homera ameiagiza RITA kuboresha mfumo wake wa kidijitali wa usajili wa Bodi za Wadhamini, kufanya mapitio ya Sheria ili ziendane na uhitaji wa sasa, kuongeza wigo wa kliniki za utoaji wa huduma ili kuwafikia wananchi huko walipo pamoja na kutoa mafunzo na usimamizi wa karibu ili kutatua changamoto za kiutendaji za bodi hizo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: