Ndugu wawili pacha wakosa kurudi shuleni
Автор: Citizen TV Kenya
Загружено: 2026-01-22
Просмотров: 846
Ndugu wawili pacha katika kijiji cha Mwachema kaunti ya Kwale wamesalia nyumbani baada ya kushindwa kujiunga na gredi ya 10.
Watoto hao wamekosa karo hata baada ya ya kufanikiwa kubadili shule walizotakiwa kujiunga nazo na kupata nafasi katika shule ya sekondari ya juu ya Kaya Tiwi. Pacha hao sasa wamelazimika kumsaidia mama yao kutafuta kuni za kuuza ili kujaribu kutafuta fedha za mahitaji ya shule na karo. Abdalla Ali Ratili aliyepata alama 48 na Hamisi Ali Ratili aliyepata alama 47 kwenye mtihani wa KJSEA wamekuwa wakipitia hali ngumu katika masomo yao.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: