Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
dTub
Скачать

Safari ya Karagwe ,Kayanga , Omurushaka

Автор: Bukobawadau Live

Загружено: 2025-02-08

Просмотров: 1248

Описание:

Safari yetu Kuelekea Wilayani Karagwe,Wilaya yenye Makao yake Makuu Kayanga na Mji wa Kibiashara 'Omurushaka.

Karagwe ni Mji wa Kihistoria wenye watu mashuhuri waliojulikana ndani na nje ya Tanzania.
CHIMBUKO/ASILI YA KARAGWE NA WATU WAKE (WANYAMBO)

Kutokana na simulizi za wazee na watafiti mbalimbali kama vile Katoke (1975; 162) jina ‘Karagwe’ jina linatokana na kilima kinachopatikana Kusini Magharibi ya Makao makuu ya wilaya ya Karagwe ,kwenye kijiji cha Kandegesho ,kata ya Nyakakika ambacho mtawala ( Omukama ) wa kwanza alifanya kafara ya kwanza. Kwa taarifa zilizopo ni kwamba mtawala huyo alijulikana kwa jina la ‘Nono ya Malija’ kutoka ukoo wa Basiita. Na kwamba kumbukumbu hii ya "Karagwe ka Nono "inatokana na ukweli kuwa Nono alikuwa mtawala wa mwisho wa wenyeji asilia kabla ya kuondolewa madarakani na Omukama Ruhinda mtoto wa Wamara. Inasemekana kwamba Nono aliondolewa kwa ujanja bila ya misukosuko wala mapigano ya aina yoyote. Kwa kifupi hii ndio kumbukumbu yake na chimbuko la historia ya jina Karagwe.

JIOGRAFIA YA WILAYA.

Wilaya ipo kilomita 105 kutoka Manispaa ya Bukoba –Makao makuu ya Mkoa wa Kagera. Wilaya inapatikana kati ya nyuzi 1o na 2o, 20' Kusini Latitudo 30o hadi 38,30 Mashariki Longitudo. Mwinuko wa ardhi kutoka usawa wa bahari ni mita 1,500 hadi mita 1,800. Hali ya hewa kwa ujumla ni joto la wastani wa degree 26oC. Mvua zinanyesha kwa wastani wa mm 1,040 hadi 1,200 kwa mwaka, kati ya mwezi Septemba na Januari na kati ya mwezi Machi na mwezi Mei.

ENEO LA WILAYA.
Wilaya ya Karagwe ina eneo la kilomita za mraba 4,500 kati ya hizo kilomita za mraba 4,342 ni eneo la nchi kavu na kilomita za mraba 158 ni eneo la maji. Eneo linalofaa kwa kilimo ni Hekta 153,540 na eneo linalolimwa ni Hekta 82,808.5 sawa na asilimia 53.9.

UTAWALA.

Kwa upande wa maeneo ya utawala, Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe ina Tarafa tano (5) ambazo ni Bugene, Nyakakika, Nyaishozi, Nyabiyonza na Kituntu. Pia wilaya ina kata 23, vijiji 77 na vitongoji 612 ambapo kati ya vitongoji hivyo 612, vitongoji 20 vipo katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kayanga na vinaitwa vitongoji kwa sababu bado mamlaka hiyo ya mji mdogo haijawa mamlaka kamili ili vitongoji hivyo viitwe mitaa. Halmashauri ya wilaya ina waheshimiwa madiwani 32 ambapo kati yao 23 ni wa kuchaguliwa kutoka katika kata za Halmashauri ya Wilaya, 8 ni wa viti maalum na mbunge wa Jimbo 1.

SHUGHULI ZA KIUCHUMI:

1. KILIMO, USHIRIKA NA UMWAGILIAJI:

Kilimo ni mojawapo ya shughuli za kiuchumi inayochangia wastani wa asilimia 70 ya pato la Halmashauri. Kaya zinazoshiriki katika shughuli za kilimo ni 61,351 kati ya kaya zote 76,425 za wilaya ya Karagwe. Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 153,540 kati ya hekta 4,500,000 ya eneo lote la wilaya. Eneo linalofaa kwa kilimo cha Umwagiliaji ni hekta 4,500 Pia Wilaya inashirikiana na wadau mbalimbali waliopo wilayani katika kuendeleza sekta ya kilimo. Baadhi ya wadau hao ni ELCT, Karagwe Agribusiness, MAVUNO, CHEMA, WORLD VISION, MATUNDA MEMA, BISHESHE WINE, KARAGWE ESTATE LTD, RADIO KARAGWE, RADIO FADECO, LUKALE WINE, KDCU, Matunda MEMA, KADERES NA OLAM.

Aidha zipo SACCOS 31 zenye jumla ya wanachama 46,319 na Chama 1 kikuu cha Ushirika (KDCU) kinachojishughulisha na ununuzi wa mazao ya wakulima. Wilaya imeanzisha na kujenga mradi mmoja mkubwa wa Umwagiliaji (Mwisa Irrigation Scheme) wenye ukubwa wa Hekta 120.

KAYA MASHUHURI

Miongoni mwa Watu Mashuhuru wapambanaji wa Karagwe toka enzi hizo Akina Giligori Byonabushs ,Familia ya Simon Kabagambi, Mfanyabiashara Maarufu pale Omurushaka Hajji Essau,Familia ya Kina Chipukizi ,AMRI Chipukizi Chimbuko la Baba mzazi wa Rafiki yetu Mnec Kharim Amri na Kina Bin Said Na wengine wengi bila kusahau Tindamanyile.

2. UFUGAJI NA UVUVI:
Wilaya ya Karagwe ina hekta 140,000 zinazofaa na hutumika kwa shughuli za ufugaji. Sekta hii uchangia kwa zaidi ya 10% katika ajira ya wananchi na pato la kaya. Mifugo ambayo hufugwa ni pamoja na ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, kuku, bata na sungura.

Shughuli za Uvuvi ufanyika katika maziwa madogo ya Burigi, Rwakajunju, Kamakala na mto Kagera. Wilaya inayo mabwawa ya kuchimbwa 67 kwa ajili ya ufugaji wa samaki. Aina za samaki wanaozalishwa kwa wingi ni sato/ngege, kambale mamba, kambale mumi, furu, ningu, soga na domodomo.

3. VIWANDA NA BIASHARA:

Mji wa Kayanga na Omurushaka pamoja na miji midogo ya Kihanga, Nyakaiga, Rwambaizi, Nyaishozi, Chanyamisa, Nyabiyonza, Nyakabanga na Ihembe ni kati ya miji inayokua kibiashara na yenye mwingiliano mkubwa wa shughuli za kiuchumi na kijamii. Maeneo haya yanaendelea kuwekeza katika viwanda vya biashara kama vile viwanda vya kukoboa Kahawa, viwanda vya kusindika maziwa, asali, kusaga na kukoboa nafaka. Shughuli za uzalishaji zinaendelea kuimarika na kuongeza uzalishaji, kupanua ajira, kukuza biashara ya uuzaji na ununuzi wa mazao tarajiwa na hivyo kuongeza kipato na kukuza uchumi, kuboresha maisha ya jamii, kupunguza umaskini wa kipato na hivyo kuchochea kasi ya kuondoa umaskini.

Safari ya Karagwe ,Kayanga , Omurushaka

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео mp4

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио mp3

Похожие видео

Karagwe kagera : Historia ya wanyambo na mfalme #rumanyika

Karagwe kagera : Historia ya wanyambo na mfalme #rumanyika

KABILA LA WANYAMBO NA TAMADUNI ZAO,NGOMA NA VYAKULA.

KABILA LA WANYAMBO NA TAMADUNI ZAO,NGOMA NA VYAKULA.

Rich African villages you never see! This is Muleba Tanzania East Africa

Rich African villages you never see! This is Muleba Tanzania East Africa

UTAPENDA BASHUNGWA ALIVYOSIMAMISHA MSAFARA AMSALIMIE RAFIKI YAKE WA KIJIJINI KWAO.

UTAPENDA BASHUNGWA ALIVYOSIMAMISHA MSAFARA AMSALIMIE RAFIKI YAKE WA KIJIJINI KWAO.

Невидимая Империя 7 тайн армянского народа, которые объясняют всё

Невидимая Империя 7 тайн армянского народа, которые объясняют всё

Посмотрите эти улицы ILALA в Дар-эс-Саламе, Танзания 🇹🇿

Посмотрите эти улицы ILALA в Дар-эс-Саламе, Танзания 🇹🇿

KUMBE WA RWANDA NI WATANZANIA, MSIKILIZE PROF KABUDI HAPA, TUNAINGILIANA MAKABILA NA NCHI 8

KUMBE WA RWANDA NI WATANZANIA, MSIKILIZE PROF KABUDI HAPA, TUNAINGILIANA MAKABILA NA NCHI 8

Goma ville touristique by Niyigena Emmanuel 2022

Goma ville touristique by Niyigena Emmanuel 2022

DRONE FOOTAGE ;KARAGWE DISTRICT COUNCIL

DRONE FOOTAGE ;KARAGWE DISTRICT COUNCIL

Лев Сбежал из Зоопарка. Все Разбежались, Кроме Одной Старушки. Вы Не Поверите, Что Было Дальше!

Лев Сбежал из Зоопарка. Все Разбежались, Кроме Одной Старушки. Вы Не Поверите, Что Было Дальше!

Tanzania karagwe omurushaka 2017

Tanzania karagwe omurushaka 2017

Masisi yacu by Niyigena Emmanuel 2021

Masisi yacu by Niyigena Emmanuel 2021

WAZIRI BASHUNGWA AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA ZAHANATI KANOGO, MILIONI 46 ZAKUSANYWA

WAZIRI BASHUNGWA AONGOZA HARAMBEE YA UJENZI WA ZAHANATI KANOGO, MILIONI 46 ZAKUSANYWA

Rich African villages you never see! This is Kamachumu Kagera Tanzania

Rich African villages you never see! This is Kamachumu Kagera Tanzania

#TAZAMA| NEEMA ILIVYOWASHUKIA WAKAZI WA KARAGWE, WAMTAJA RAIS SAMIA

#TAZAMA| NEEMA ILIVYOWASHUKIA WAKAZI WA KARAGWE, WAMTAJA RAIS SAMIA

MNEC Kagera Atembelea Kituo cha Hija Rudi Bugene/Historia ya Sisimua

MNEC Kagera Atembelea Kituo cha Hija Rudi Bugene/Historia ya Sisimua

Кровь СЛАВЯН, имя ТЮРКОВ… Но ДНК болгар раскрыло ТРЕТЬЮ тайну, которую скрывали веками!

Кровь СЛАВЯН, имя ТЮРКОВ… Но ДНК болгар раскрыло ТРЕТЬЮ тайну, которую скрывали веками!

⚡️ Зеленский запросил переговоры с Путиным || Срочная эвакуация в Украине

⚡️ Зеленский запросил переговоры с Путиным || Срочная эвакуация в Украине

Bukoba Tanzania 2025! They call it Rio De Janeiro of Africa

Bukoba Tanzania 2025! They call it Rio De Janeiro of Africa

Urubyiruko rw’Abanyekongo ruba mu mahanga rwatangiye gusura iwabo!

Urubyiruko rw’Abanyekongo ruba mu mahanga rwatangiye gusura iwabo!

© 2025 dtub. Все права защищены.



  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности



Контакты для правообладателей: [email protected]