JIANDAE MKE WA RAIS MWINYI ATOA TAARIFA MUHIMU ZANZIBAR
Автор: Tifu Tv
Загружено: 2024-12-04
Просмотров: 2448
MKE wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mama Mariam Mwinyi ametoa wito kwa wazazi na walezi majumbani, kuitumia fursa iliyopo kwa kuwapeleka Skuli zilizokaribu na maeneo yao wanayoishi, watoto wote waliokuwa na sifa ili waandikishwe.
Mama Mariam Mwinyi ametoa wito huo alipozungumza na wazazi na walezi kupitia taarifa aliyoitoa kwa umma akiwa Ofisini kwake Ikulu ya Migombani, Mkoa wa Mjini Magharibi kuhusu zoezi la uandikishwaji wanafunzi wa ngazi ya maandalizi na msingi kwa mwaka wa masomo 2025 kwa skuli zote za Serikali na binafsi.
Ameiagiza jamii watoto wote waliofikia umri wa miaka 4 hadi 5 waandikishwe kwa ngazi ya Maandalizi na watoto wote watakaofika umri wa miaka 6 ifikapo mwaka 2025 waandikishwe kwa ngazi ya Msingi.
Mama Mariam Mwinyi ambae pia ni Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya “Zanzibar Maisha Bora Foundation” (ZMBF), aliwahimiza wazazi na walezi kuhakikisha wanawachukulia vyeti vya kuzaliwa watoto wao wanapokwenda kuwaandikisha.
“Ndugu Mzazi, hakikisha unapokwenda Skuli kumuandikisha mtoto wako usisahau kuchukua cheti chake cha kuzaliwa”. Mama Mariam Mwinyi alihimiza.
Aidha, Mama Mariam alisema kwa sasa zoezi la uandikishaji kwa Skuli zote za Serikali na Binafsi linaendelea nchini kote mpaka tarehe 30/12/2024.
Pia, ametoa wito kwa wazazi na walezi kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi za kuwawekea miundombinu wezeshi ya elimu kwa kuwapeleka watoto wote kuandikishwa na kuhakikisha hakuna mtoto atakayebakia nyumbani.
Mama Mariam amesisitiza kazi ya uandikishaji ni kwa watoto wetu wote hauchagui, jinsia au wenye ulemavu.
Amesema, kwa Skuli za Serikali watoto wote wataandikishwa bila ya gharama yoyote kwani elimu ni haki ya Msingi kwa kila mtoto.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: