Mfumuko wa Bei za Chakula Wapanda Zanzibar – Desemba 2025
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-01-14
Просмотров: 480
Kiwango cha mfumuko wa bei za chakula kwa kipindi cha miezi 12 hadi kufikia mwezi wa Disemba 2025 kimefikia asilimia 3.81, kikiongezeka kutoka asilimia 3.34 iliyorekodiwa mwezi Novemba 2025.
Tathmini hiyo imetolewa na Mtakwimu wa Kitengo cha Bei, Ndugu Hassan Jamal Hassan, kutoka Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Zanzibar, iliyopo Mazizini, Wilaya ya Mjini Unguja.
Ameeleza kuwa ongezeko hilo limetokana na kupanda na kushuka kwa bei za vyakula mbalimbali, akitaja baadhi ya bidhaa zilizochangia kuongezeka kwa mfumuko wa bei kuwa ni pamoja na ndizi za mkono mmoja, mchele wa Mbeya, samaki, mafuta ya kupikia, ndizi mtwike, mkate wa boflo, gesi ya kupikia, mafuta ya dizeli pamoja na mafuta ya petroli.
Kwa niaba ya wafanyabiashara wa ndizi katika Soko la Kibandamaiti, Ndugu Mohd Hakim Juma amesema kuwa ongezeko la bei za ndizi linasababishwa na changamoto za usafiri, hususan ucheleweshaji wa usafirishaji wa ndizi kutoka Kisiwa cha Pemba kwenda Unguja.
Aidha, ameiomba Serikali kupunguza ushuru kwa wasafirishaji wa ndizi, akieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kupunguza bei ya bidhaa hizo sokoni na kuwasaidia wananchi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: