Ajali Same: Ndugu wa marehemu watakiwa kwenda kuchukuliwa DNA
Автор: UTV Tanzania
Загружено: 2025-06-29
Просмотров: 4587
Mamlaka za Serikali wilayani Same mkoani Kilimanjaro zimewataka ndugu wa marehemu wa ajali ya jana,Jumamosi, Juni 29,2025 kufika katika Hospitali ya KCMC kwa ajili ya uchukuaji wa sampuli za vinasaba (DNA) ili kusaidia utambuzi wa miili ya wapendwa wao iliyoungua vibaya kwenye ajali hiyo.
Ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 38 na majeruhi 29, ambapo hadi sasa 27 kati ya majeruhi hao wameruhusiwa kurejea nyumbani. Tukio hilo lilitokea Jumamosi saa 11 jioni, baada ya basi la Kampuni ya Channel One lililokuwa likielekea Tanga kutoka Moshi kugongana uso kwa uso na basi dogo aina ya Toyota Coaster lililokuwa limebeba wanachama wa kikundi cha VICOBA waliokuwa safarini kuelekea kwenye harusi ya mtoto wa mwenzao.
Ajali hiyo ilifuatiwa na mlipuko wa moto ulioteketeza magari yote mawili.
#azamnewsupdates
✍Enosi Masanja
Mhariri| @official_jennifersumi
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: