TANAPA YAKABIDHI VIAKISI MWANGA 1000 KWA MKUU WA WILAYA YA BUNDA
Автор: Adelinus Banenwa
Загружено: 2024-10-03
Просмотров: 5
TANAPA kanda ya magharibi itoa refrector 1000 kwa waendesaha pikipiki maarufu bodaboda wilayani Bunda.
Akikabidhi msaada huo kwa mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano leo Oct 3, 2024 ofisini kwakwe, Albert Mziray ambaye ni msimamizi wa kitengo cha uhifadhi na maendeleo ya biashara TANAPA kanda ya magharibi kwa niaba ya kamishna waTANAPA kanda hiyo mziray amesema wameamua kufanya hivyo ili kusaidia vijana kuepukana na ajari.
Mziray ameongeza kuwa msaada huo ni sehemu ya ujirani mwema ambapo TANAPA wamekuwa wakitoa kwa jamii inayozunguka hifadhi na misaada hiyo ni muendelezo.
Akipokea msaada huo mkuu wa wilaya ya Bunda DKT Vicent Naano amewashukuru TANAPA kwa kuwa na moyo wa kujitoa kusaidia jamii huku akibainisha kuwa huo ndiyo umuhimu wa kuwa na wanyamapori na hifadhi karibu.
Dc Naano amesema TANAPA wamesaidia kwa kiasi kikubwa katika shughuli za maendeleo katika jamii ikiwemo utengenezaji madawati, ujenzi wa zahanati, madarasa miongoni mwa kazi zingine.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: