Wanafunzi wa chuo cha Nairobi wafika ofisi za HELB
Автор: Citizen TV Kenya
Загружено: 2025-02-03
Просмотров: 1213
Baadhi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi wamevamia ofisi za bodi ya utoaji mikopo ya wanafunzi za HELB wakilalamikia kuchelewa kwa mikopo yao
Wanafunzi hawa waliokita kambi nje ya jumba la Anniversary wamelalamikia kushindwa kugharamia mahitaji yao ya elimu na kibinafsi kutokana na kuchelewa kwa mikopo hii. Polisi walilazimika kushika doria kuzuia ghasia. Baadaye wawakilishi wa wanafunzi waliruhusiwa kuingia ndani ambako maafisa wa HELB waliwaahidi kuwa wangepata malipo yao kufikia mwisho wa siku ya leo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: