NENO LA SIKU | Mathayo 26 | Maombi Ya Kuvunja Maagano Ya Damu | Isaac Javan
Автор: Neno La Siku
Загружено: 2024-03-15
Просмотров: 10336
Leo tunasoma kitabu cha Mathayo sura ya ishirini na sita, na tunaenda kufanya maombi ya kuvunja maagano ya damu. Katika ulimwengu wa roho, damu ni kitu kikubwa sana kinachotumika kufunga au kufungua maisha ya mtu.
Shetani anaufahamu ukweli huo, na ndiyo maana moja ya mbinu anazotumia kufunga maisha ya watu ni kuwaingiza kwenye maagano ya damu. Vifungo vya maagano ya damu ni aina ya vifungo vyenye uwezo wa kuathiri kizazi kimoja mpaka kingine.
Lakini upo ushindi ndani ya YESU na kupitia maombi ya leo tunaenda kufanya maombi ya kuvunja maagano ya damu ili yasiweze kukufutilia tena na kukutesa. Kwa hiyo utakapoingia katika maombi ya leo, ninakushauri uombe pamoja na mimi kwa kumaanisha, na utauona mkono wa BWANA ukikushindia.
Damu ya YESU inayonena mema inene mema kwa ajili yako na kukuvusha katika siku ya leo. Mungu akubariki sana na akupe mwanzo mpya wa maisha yenye amani, ushindi, na furaha katika Roho Mtakatifu. Amen
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: