NENO LA SIKU | Mathayo 27 | Maombi Ya Kushinda Dharau | Isaac Javan
Автор: Neno La Siku
Загружено: 2024-03-19
Просмотров: 5237
Leo tunasoma kitabu cha Mathayo sura ya ishirini na saba, na tunaenda kufanya maombi ya kushinda dharau. Moja kati ya mambo yanayoharibu maisha ya watu na kuwafanya wakate tamaa ni dharau.
Inawezekana kwenye maisha yako umewahi kudharauliwa. Au inawezekana wazazi wako wamewahi kudharauliwa. Ni moja kati ya uzoefu mbaya ambao shetani anautumia kukwamisha na kuharibu maisha ya watu.
Lakini YESU analo jibu la nini tunatakiwa kufanya pale tunapodharauliwa na watu. Na siku ya leo tunaenda kufanya maombi maalum kwa ajili ya kushinda dharau zinazotoka kwa watu wengine na kuelekezwa kwetu.
Nami nakuombea YESU akupe ushindi katika maombi haya. YESU akupe heshima na akuvike vazi la sifa na utukufu. Ukauone mkono wa BWANA ukikuvusha na kukuheshimisha kwenye mambo yako yote.
Mungu akubariki sana na kukupa kibali na neema. Amen
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: