NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI AFYA ATAKA WATUMISHI KUTUMIA LUGHA YA UPOLE KWA WAGONJWA.
Автор: CLOUDS HABARI
Загружено: 2025-11-26
Просмотров: 3
NAIBU WAZIRI WA TAMISEMI AFYA ATAKA WATUMISHI KUTUMIA LUGHA YA UPOLE KWA WAGONJWA.
Naibu Waziri wa TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya afya Dkt. Jafari Rajabu Seif, amewataka watoa huduma za afya nchini kuhakikisha wanatoa huduma kwa kutumia lugha ya upole, staha na tabasamu wanapowahudumia wagonjwa.
Naibu Waziri Dkt. Jafari ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza katika Kituo cha Afya cha Nyarugusu kilichopo Kata ya Nyarugusu, Jimbo la Busanda Mkoani Geita, ambapo amesema serikali ya awamu ya sita inaendelea kufanya maboresho makubwa kwenye sekta ya afya, hivyo ni wajibu wa watumishi kuhakikisha huduma wanazotoa zinaendana na viwango vinavyotarajiwa.
“Serikali ya Dkt. Samia itaendelea kuboresha huduma za afya, ikiwemo ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vituo vya afya na zahanati. Hata hivyo, pamoja na maboresho hayo, nyinyi watoa huduma mna wajibu wa kumpokea mgonjwa kwa tabasamu na kutumia lugha safi, si lugha chafu,” amesema Dkt. Jafari.
Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa kituo hicho, Fredi Felisian, amesema ziara ya Naibu Waziri imewapa hamasa mpya, akibainisha kuwa kituo hicho kinahudumia idadi kubwa ya wananchi na kinahitaji maboresho zaidi ili kuendelea kutoa huduma bora na kwa ufanisi.
#CloudsDigtalUpdates.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: