SERIKALI IMETOA BIL 424.6 UTEKELEZAJI MIRADI YA TANRODS RUKWA-ENG MWANGA
Автор: WazoHuru Media
Загружено: 2025-10-20
Просмотров: 49
Katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa zaidi ya shilingi bilioni 424.6 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Kitaifa ikiwemo Ukarabati wa uwanja wa Ndege Sumbawanga na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami. Aidha, kuna kazi za Matengenezo ya barabara pamoja na kazi za dharura zilizotekelezwa zikijumuisha miradi ya usanifu wa Barabara za TANROADS mkoa wa Rukwa.
Mkoa wa Rukwa una mtandao wa Barabara wa kilometa 1250.84, katika mtandao huo, Barabara kuu ni kilometa 415.86 na Barabara za mkoa ni kilometa 834.98 kati hizo barabara kuu za lami ni Kilometa 298.35 na Barabara kuu changarawe ni kilometa 117.51. Kwa upande wa Barabara za Mkoa kiwango cha lami ni kilometa 76.83 na Barabara za mkoa Changarawe ni Kilometa 758.15.
Akizungumza ofisi kwake Mjini Sumbawanga leo tarehe 20 Octoba 2025 Meneja wa TANROADS Mkoa wa Rukwa Mhandisi Mgeni Mwanga amesema kuwa serikali inaendelea na ukarabati na uboreshaji wa uwanja wa ndege wa Sumbawanga ambao umefikia asilimia 86 na unajengwa na mkandarasi Beijing Construction Engineering Group Co Ltd chini ya Mhandisi Mshauri SMEC International kwa ushirikiano na SMEC Tanzania Ltd chini ya ufadili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya kwa gharama ya shilingi bilioni 60.1
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: