Uongozi wa Hospitali yataja sababu kuchanganya miili ya marehemu, Ndugu watoa ya moyoni
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2023-06-30
Просмотров: 3533
Moshi. Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi, umesema mkanganyiko uliotokea wa kuchanganya miili ya marehemu, ulitokana na marehemu Idd Semindu wa Chalinze, kutokuwa na ndugu Moshi, hivyo waliotumwa kuandaa na kuchukua mwili, kushindwa kufanya utambuzi sahihi.
Hatua hiyo ilisababisha usumbufu kwa ndugu wa Massawe walipofika kuandaa mwili na kuuchukua kwenda kuzika, jambo ambalo lililazimu uongozi wa Hospitali kwa kushirikiana na ndugu, kwenda hadi Chalinze kuufukua mwili ambao ulishazikwa toka jumatatu na kuurudisha kuzikwa upya Kibosho.
Juni 26 mwaka huu, ulichukuliwa mwili wa Steven Massawe wa Kibisho Mkombole, Wilaya ya Moshi, na kwenda kuzikwa Chalinze mkoani Pwani, huku mwili wa Idd Semindu ambaye ni wa Chalinze ukiachwa Mochwari.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: