MICHEZO YA KUBAHATISHA SIYO AJIRA-GBT
Автор: Khomein Tv
Загружено: 2025-08-12
Просмотров: 40
Wananchi wanaojihusisha na michezo ya kubahatisha wamehimizwa kutambua umuhimu wa kufuata taratibu pindi wanaposhiriki michezo ya kubahatisha huku wakihitajika kuongeza umakini zaidi ili kuepukana na athari mbalimbali zinazoweza kujitokeza kutokana kufanya hivyo kinyume na taratibu.
Rai hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania (GBT), DANIEL OLE SUMAYAN wakati akielezea mafanikio ya Bodi hiyo katika serikali ya awamu ya sita ambapo amesisitiza umuhimu wa kuongeza umakini na kutoifanya michezo hiyo kama chanzo rasmi cha ajira badala yake watambue kuwa ni sehemu ya burudani hivyo ni vyema kucheza kwa staha ili kuepukana na athari mbalimbali ikiwemo uraibu.
OLE SUMAYAN amewasisitiza pia wazazi na jamii kwa ujumla kuthibiti watoto wenye umri chini ya Miaka 18 kujihusisha na michezo hiyo kwani ni kinyume cha sheria kwa watoto kujihusisha na michezo hiyo.
Katika hatua nyingine, OLE SUMAYAN ameelezea mafanikio ya Bodi ambapo kwa kipindi cha miaka mitano imefanikiwa kuchangia shilingi Bilioni 53.8 kuendeleza michezo nchini na kuzalisha ajira zaidi ya 30,000 katika sekta ya michezo huku ikisajili jumla ya Kampuni 62 na kutoa leseni 8549.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Dar
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: