Je, unafurahia ndoto zako unazopata?
Автор: Kijiweni na Roho Mtakatifu tv
Загружено: 2025-10-15
Просмотров: 34
Shalom Wana na Urithi wa Mungu Baba katika Kristo Yesu mliojazwa na furaha pamoja na kicheko cha Bwana kila siku na katika kila eneo la maisha yenu.
“Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.”
Flp 4:4 SUV
Tunapenda kumshukuru Mungu kwa ajili ya mfululizo wa sehemu iliyoisha katika Kijiweni na Roho Mtakatifu. Zaidi kuwashukuru nyote ambao mnazidi kujitoa kwa kufuatilia vipindi hivi na namna mbalimbali kupitia muda wenu, ushauri, fedha, vifaa, eneo na vingine vyote. Mungu Baba na azidi kuwabariki na kuwaongeza katika mambo yote.
Mnamo mwaka 2022, tulipata neema ya kuwa na kipindi cha NDOTO, MAONO, PICHA, SAUTI, UFUNUO,RANGI Na NAMBA NDANI YA UFALME WA MUNGU. Ambapo tulishirikashana kwa namna tofauti kuona jinsi Mungu huzungumza nasi kupitia njia hizi tofauti tofauti katika kipindi hizi ikiwa ni sehemu ya ushirika naye.
Basi tumekuja tena mezani kuwaletea chakula kinono sana katika muendelezo wa somo lililopita ambapo tutawaletea ROHO WA NEEMA, UTOFAUTI NA UTAJIRI ULIOPO KATIKA NDOTO.
✅Je, unafurahia ndoto zako?
✅Je, huwa unazikumbuka ndoto zako?
✅Je, una utamaduni wa kufuatilia ndoto zako?
✅Je, umepata majibu ya ndoto zako zote?
Basi usisite kuwasiliana nasi na kutushirikisha majibu ya maswali hayo juu na pia kama kuna ndoto ndani ufalme wa Mungu hujawahi kuelewa usisite kuwasiliana nasi.
Karibu Kijiweni na Roho Mtakatifu.
Kijiwe ni kimoja tu, Kijiweni na Roho Mtakatifu.
“Tulio na Mungu, Tuna Roho wa Mungu.”
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: