MATHAYO 24: CHUKIZO LA UHARIBIFU NA NABII DANIELI/MWENYE SIKIO NA ASIKIE
Автор: SIRI ZA BIBLIA
Загружено: 2021-04-29
Просмотров: 13085
#Yesu#ChukizolaUharibifu##Danieli#Mwakasege
Basi, mtakapoona ‘Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake), 16hapo, walioko Yudea na wakimbilie milimani. 17Aliye juu ya paa la nyumba yake asishuke kuchukua kitu nyumbani mwake. 18Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake. 19Ole wao kina mama waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo! 20Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe siku za baridi au siku ya Sabato! 21Maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa ulimwengu mpaka leo, wala haitapata kutokea tena. 22Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa.
23“Basi, mtu akiwaambieni siku hizo: ‘Kristo yuko hapa’ au ‘Yuko pale,’ msimsadiki. 24Maana watatokea akina Kristo wa uongo na manabii wa uongo. Watafanya ishara kubwa na maajabu ya kuweza kuwapotosha ikiwezekana hata wateule wa Mungu. 25Sikilizeni, nimekwisha waonya kabla ya wakati. 26Basi, wakiwaambieni, ‘Tazameni, yuko jangwani,’ msiende huko; au, ‘Tazameni, amejificha ndani,’ msisadiki; 27maana, kama vile umeme uangazavyo toka mashariki hadi magharibi, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu. 28Pale ulipo mzoga, ndipo watakapokusanyika tai.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: