MKUU WA MKOA MJINI MAGHARIBI ASISITIZA USHIRIKIANO NA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MANISPAA MJINI
Автор: MANISPAA MJINI ONLINE TV
Загружено: 2026-01-16
Просмотров: 45
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Mheshimiwa Moh'd Ali Abdalla, amewataka watendaji wa Baraza la Manispaa Mjini Madiwani pamoja na Masheha wa Wilaya ya mjini kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku ili kuongeza ufanisi na kuharakisha maendeleo ya Manispaa.
Mheshimiwa Abdalla ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza katika kikao maalum kilichofanyika katika katika ukumbi wa skuli ya Haile selassie Mjini Unguja.
Amesema kuwa ushirikiano wa dhati kati ya wadau hao ndio msingi na suluhisho la changamoto nyingi zinazojitokeza katika utendaji wa kazi za Serikali katika ngazi ya jamii.
Aidha Mkuu wa Mkoa alisisitiza umuhimu wa kuimarisha usafi wa mazingira na kupendezesha Mji huku akiagiza Baraza la Manispaa kuanzisha utaratibu wa kufanya usafi wa pamoja mara moja kila mwezi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: