BAA LA NJAA SAME!: KIJIJI KILICHOATHIRIWA NA MAFURIKO, WAMTUPIA LAWAMA MWENYEKITI KUWATENGA.
Автор: Ndc Online Media
Загружено: 2025-07-24
Просмотров: 383
Kamati ya Usalama Wilaya ya Same imesisitiza kuwa uamuzi wa kutoa mashamba yenye ukubwa wa hekari 260 kwa muda kwa wakulima wapatao 600 wa Kijiji cha Marwa, ambao mashamba yao yaliathiriwa na mafuriko tangu Mei, umelenga kukabiliana na hatari ya baa la njaa kutokana na wakazi hao kukosa maeneo ya kulima kwa zaidi ya miezi minne.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Same, Mhe. Kasilda Mgeni, ameeleza hayo Julai 21, wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo kufuatilia hatua zilizochukuliwa na serikali baada ya mvua kubwa kusababisha uharibifu wa mali, ikiwa ni pamoja na mashamba.
“Tusingeweza kuwaacha wakulima zaidi ya 600 pamoja na familia zao waendelee kukosa maeneo ya kilimo. Mkumbuke suala la njaa ni la kiusalama. Tulitembelea maeneo yote mawili, lile lililoathirika na jingine ambalo wakulima waliomba walitumie kwa muda. Baada ya kufanya mkutano na wananchi na kufikia makubaliano, wakulima hao walianza kupewa eneo mbadala kwa mujibu wa makubaliano hayo,” alisema Mhe. Kasilda.
Hata hivyo, amefafanua kuwa wakati wa kugawa mashamba hayo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Marwa hakushiriki na alikaidi maagizo halali ya serikali. Aidha, anadaiwa kuunda kikundi cha wafugaji wa jamii ya Kimasai kwa lengo la kuvuruga utekelezaji wa ugawaji huo, huku wakiondoa alama za mipaka ya mashamba yaliyokuwa yameanza kugawiwa. Inadaiwa Mwenyekiti huyo ameegemea upande wa wafugaji na kuwabagua wakulima.
Baadhi ya wakulima wameeleza kuwa mwenyekiti huyo ndiye chanzo cha migogoro kati yao na wafugaji, akipinga maagizo ya Mkuu wa Wilaya na kuwatumia wafugaji hao kupinga mchakato wa ugawaji wa mashamba mbadala.
“Tunashangazwa na mwenyekiti wetu. Ameleta mgawanyiko mkubwa hapa kijijini na sasa ameegemea upande wa wafugaji kwa sababu naye ni mfugaji. Sisi wakulima tumetengwa na anapinga maagizo ya Mkuu wa Wilaya aliyoyakubali mwenyewe kwenye mkutano wa awali,” alisema mmoja wa wakulima hao.
Waandishi wa habari walijaribu kumtafuta Mwenyekiti wa Kijiji cha Marwa bila mafanikio, licha ya awali kuahidi kufika eneo hilo na wafugaji. Hata hivyo, simu zake hazikupatikana na badala yake walifika wakulima ambao waliendelea kueleza changamoto zao.
Kwa sasa Mwenyekiti huyo anakabiliwa na kesi mbalimbali, ikiwemo kesi ya kutishia kuua kwa maneno (Kesi Na. 52 ya mwaka 2025) na kesi nyingine ni Shambulio la kawaida (Na. 54 ya mwaka 2025) inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mhe. Merina Kidesi katika Mahakama ya Mwanzo Same.
Serikali imewasihi wananchi hao kuwa watulivu huku hatua za kushughulikia changamoto hizo zikiendelea. Kijiji cha Marwa kina wakazi ambao ni wakulima na wafugaji, ambao wanaishi ndani ya Pori Tengefu la Same-Ruvu upande wa kata ya Ruvu kwa masharti maalum, ikiwemo kutoanzisha kilimo cha kudumu au maeneo mapya kwa sasa wakati wakisubiri maelekezo ya Kamati Maalum ya Mawaziri Wanane wa Kisekta.#malawi #ccm #azamm #chadema #africa #simba #crossfit #kilimanjaro #kilimanjarosafari #moshi
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: