MILA, DESTURI POTOFU ZINAVYOCHANGIA UDUMAVU KATAVI
Автор: Daily News Digital
Загружено: 2026-01-19
Просмотров: 54
KATAVI: BAADHI ya mila na desturi zinazofanywa na makabila mkoani Katavi zimetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochangia tatizo la udumavu, hali iliyowafanya wananchi kuiomba Serikali kuongeza elimu ya lishe ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Wakizungumza kuhusu suala hilo, wananchi wamesema kuwa mabadiliko ya fikra na mitazamo potofu yatasaidia kuachana na baadhi ya mila zinazoathiri afya, hususan zile zinazohusisha imani za kishirikina. Imani hizo, kwa baadhi ya jamii, hupelekea kubagua au kukataza ulaji wa vyakula fulani vyenye virutubisho muhimu, ikiwemo mayai kwa kinamama wajawazito na watoto wadogo.
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo, hali ya udumavu mkoani Katavi imefikia asilimia 32.2. Kutokana na hali hiyo, mkoa umeweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuongeza juhudi za uelimishaji wa lishe, kufanya tafiti za kina kubaini chanzo halisi cha tatizo, pamoja na kuchukua hatua madhubuti za kulikabili.
Akizungumza katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa lishe ngazi ya mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko, amesisitiza kuwa kila kiongozi anatakiwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kusimamia na kufuatilia mipango iliyowekwa na mkoa katika mapambano dhidi ya tatizo la udumavu.
Ameongeza kuwa ushirikiano kati ya viongozi, wataalamu wa afya na wananchi ni muhimu ili kufanikisha azma ya kupunguza na hatimaye kutokomeza udumavu mkoani Katavi.
Follow us on:
FACEBOOK;
SpotiLeo: / spotileo-176. .
HabariLeo: / habarileo
DailyNews: / dailynewstz
INSTAGRAM;
HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig...
SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid...
TWITTER;
Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: