BUTIKU: HATA MIMI SIJUI POLEPOLE ALIPO, MSINIULIZE...
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2026-01-19
Просмотров: 104
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku amesema kabla ya kujiuzulu, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole alikutana naye mara mbili kumweleza matatizo yake.
Butiku amebainisha hayo leo, Jumatatu Januari 19, 2026, katika mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu kikao cha wazee, Butiku ameweka wazi kuwa yeye ni miongoni mwa waliofuatwa na Polepole mara mbili kabla ya kujiuzulu.
Amesema mara ya kwanza, Polepole alimfuata na kumweleza changamoto zake za kazi alipokuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi, kabla hajahamishiwa Cuba.
“Mara ya pili akaja akasema kusiwe na uchaguzi, nikamwambia kama hakuna uchaguzi hamtakuwa na Rais, kama huna Rais nani ataongoza nchi yenu, hatukukubaliana akaenda,” amesema.
Mara ya tatu, amesema hawakukutana bali alimpigia simu na kumweleza kwamba, kama ajenda ya kutofanyika uchaguzi haitakuwepo, anaona bora aache kazi (ya ubalozi wa Cuba).
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: