KUONGEZA MUDA WA UDAHILI WA SHAHADA YA KWANZA KATIKA PROGRAMU ZENYE NAFASI MWAKA WA MASOMO 2024/2025
Автор: TCU TV Tanzania
Загружено: 2024-10-04
Просмотров: 3247
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) leo Oktoba 04, 2024 imetangaza kuongeza muda wa udahili wa Shahada ya Kwanza katika programu ambazo bado zina nafasi kwa mwaka wa masomo 2024/2025.
Akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Makao Makuu ya TCU Jijini Dodoma, Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa amesema kuwa Awamu ya Tatu na ya mwisho ya udahili itaanza tarehe 05 hadi 09 Oktoba 2024. Aidha, amewaasa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika Awamu ya Pili kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hiyo vizuri kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda.
Katibu Mtendaji amevielekeza Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi.
Vile vile, Profesa Kihampa amebainisha kuwa Awamu ya Pili ya udahili kwa mwaka wa masomo 2024/2025 imekamilika. Majina ya waliodahiliwa katika awamu hiyo yatatangazwa na vyuo husika tarehe 05 Oktoba, 2024.
Kwa wale waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Pili ya udahili na wale ambao hawakuweza kuthibitisha udahili katika Awamu ya Kwanza, Profesa Kihampa amesema kuwa wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia tarehe 05 hadi 21 Oktoba, 2024.
Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili. Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanapaswa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: